Mama Maria Nyerere, amempongeza Katibu Mkuu wa CCM, kwa juhudi kubwa ambazo anaendelea kuzifanya za kumsaidia Mwenyekiti wa Chama Rais Dk. John Magufuli katika kurejesha Chama na Serikali kwenye misingi ambayo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, aliisimamia.
Katika mazungumzo, Mama Maria kwa umahususi na kwa kupitia kwa Dk. Bashiru amempongeza Rais Dk. Magufuli kwa kazi nzuri ya ujenzi wa vituo vya afya zaidi ya 200 kote nchini Tanzania ndani ya kipindi kifupi cha miaka miwili, vituo ambayo vina huduma ya afya timilifu (comprehensive health care).
Mama Maria ameeleza vituo hivi vitakuwa mkombozi wa upatikanaji wa huduma za afya hasa kwa mama, watoto na wazee.
Katika mazungumzo hayo Mama Maria ametoa mwito kwa CCM kuendelea kuisimamia Serikali na kuimarisha lishe bora kwa watoto, watu wazima na umma ili kujenga Taifa imara na la watu wenye nguvu ya kuendelea kuchapa kazi sambamba na kauli mbiu ya Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu!
Akipokea pongezi hizo Dk. Bashiru Ally, amemshukuru Mama Maria kwa kuendelea kuwajali, kuwakumbusha, kuwashauri na kuwaombea viongozi kila anapopata nafasi.
Dk. Bashiru amemjulisha Mama Maria kwamba tarehe 17 na 18 Desemba kutafanyika vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Halmashauri Kuu ya Taifa ambapo serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitatoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Mwaka 2015 - 2020.
Taarifa iliyolewa na Idara ya Itikadi na Uenezi imesema mazungumzi hayo ni mwendelezo wa ziara na mazungumzo ya Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally na viongozi, makada na wanachama wa CCM ili kupokea ushauri, kubadilishana nao uelewa, mipango, mikakati na taarifa za ujenzi wa Chama.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇