Mar 29, 2025

WASIRA AWAHAKIKISHIA WAKULIMA, CCM KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO

  MAKAMU Mwenyekiti wa Chana Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amewahakikishia wananchi wilayani Kishapu, Mkoa wa Shinyanga Chama hicho kitaendelea kutatua changamoto zao ikiwemo ya kuhakikisha wanapata mazao mengi ya kilimo kwa kusambaza pembejeo na kujenga miundombinu muhimu.


Wasira ameeleza hayo Machi 28, 2025 alipokuwa akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM wilayani humo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 na kusikiliza changamoto za wananchi pamoja na kuhutubia mikutano ya hadhara mkoani Shinyanga.

Wasira alihitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani Shinyanga na kuanza ziara kama hiyo mkoani Simiyu.






No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages