Oct 21, 2018

MAREKANI NA NIA YAKE YA KUJIONDOA KWENYE MKATABA WA SILAHA ZA NYUKLIA ZA MASAFA YA KATI

Miongoni mwa nyanja muhimu za mivutano ya mara kwa mara baina ya Russia na Marekani hususan katika kipindi cha utawala wa Rais Donald Trump wa nchi hiyo ni masuala ya kijeshi na silaha. Hivi sasa na baada ya Marekani kujiondoa katika mikataba kadhaa ya kimataifa kumeongezeka wasiwasi kwamba, yumkini nchi hiyo ikajiondoa pia katika baadhi ya mikataba wa silaha.
Habari zinasema kuwa, maafisa wa serikali ya Marekani wametoa wito wa kujiondoa nchi hiyo katika mkataba ya wa silaha za nyuklia za masafa ya kati (INF) kutokana na hitilafu zilizopo baina ya nchi hiyo na Russia. Katika uwanja huo Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani, John Bolton amemtaka Rais Donald Trump wa nchi hiyo ajiondoe katika mkataba huo. Bolton pia anakusudia kuzuia mazungumzo juu ya suala la kuongezwa muda wa mapatano ya kupunguza silaha za nyuklia ya START yaliyotiwa saini na nchi hizo mbili mwaka 2010. 
Japokuwa inasemekana kuwa, pendekezo hili la John Bolton limepingwa vikali na Wizara za Mashauri ya Kigeni na Ulinzi za Marekani lakini gazeti la New York Times limevichua kuwa, serikali ya Trump inajitayarisha kujiondoa katika mkataba wa silaha za nyuklia za masafa ya kati. Trump anataka kuiondoa Marekani katika mtaba huo kwa kisingizio kwamba, Russia imeukiuka na kwa sababu mtakaba huo unaizuia Marekani kutengeneza silaha mpya za kukabiliana na makombora ya China huko mashariki mwa Asia. Habari zinasema katika safari yake ya wiki ijayo mjini Moscow, Bolton atamtaarifu Rais Vladimir Putin wa Russia kuhusu azma ya Marekani ya kujiondoa katika mkataba huo. 
John Bolton
Iwapo Marekani itajiondoa katika mkataba huo wa INF, huo utakuwa mkataba wa kwanza muhimu wa kudhibiti silaha kutupiliwa mbali na kukanyagwa na Donald Trump. Katika kipindi cha miaka minne iliyopita Marekani imekuwa ikiituhumu Russia kuwa inakiuka mkataba huo. Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama hakuthubuti kuiondoa nchi hiyo katika mkataba huo muhimu licha ya kwamba alikuwa akiikosoa Russia kwamba inaukiuka. 
Nchi hizo mbili zimekuwa zikituhumiana kukiuka mkataba huo. Mkataba INF ulitiwa saini mwaka 1987 mjini Washington na kuanza kutekelezwa mwaka 1988. Mkataba huo wa silaha za nyuklia za masafa ya kati unazizuia nchi hizo mbili kuweka makombora ya balestiki na ya Cruise barani Ulaya. Mkataba huo pia unasisitiza ulazima wa kuharibiwa makombora ya nyuklia ya masafa ya kati ya kilomita 1000 mpaka 5500 na yale ya masafa mafupi ya kilomita 500 hadi 1000. 
Kwa kutumia kisingizio kwamba, Russia imekiuka makubaliano ya nyuklia ya masafa ya kati, Marekani imeiwekea vikwazo Moscow na imetishia hata kuishambulia Russia. Balozi wa kudumu wa Marekani katika Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) Kay Bailey Hutchison ameituhumu Russia kuwa inastawisha kwa siri mfumo wa makombora yaliyopigwa marufuku ya Cruise na kutishia kwamba, Washington itashambulia na kuharibu mfumo huo kabla haujaanza kufanya kazi. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova amepinga madai hayo na kusema kuwa: Inaonekana kwamba watu wanaotoa matamshi kama haya hawaelewi kiwango cha majukumu yao na na hawajui hatari ya lugha yao ya hujuma. Moscow pia imesema mpango wa Marekani wa kupeleka mabomu mapya ya nyuklia ya B12-16 huko Ulaya ni ukiukaji wa makubaliano ya INF.
Image Caption
Inaonekana kuwa, mivutano na hitilafu za Marekani na Russia zinazielekeza pande hizo mbili katika makabiliano ya moja kwa moja ya kijeshi au vita baina ya nchi hizo mbili zinazomiliki silaha za nyuklia. Kuhusu suala hilo Rais Vladmir Putini anasema: Iwapo nchi yoyote itaishambulia Russia kwa silaha za nyuklia suala hilo litakuwa na maana ya kumalizika maisha ya kiumbe mwanadamu katika sayari ya dunia na watakaofanya hujuma hiyo wanapaswa kuelewa kwamba watapata adhabu kali.  

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages