Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa treni mpya za SGR maarufu kama Mchongoko wameshazipa majina ya viongozi pamoja na maeneo maarufu nchini ikiwemo Serengeti Express na Mji Mkongwe Express. Tayari treni 10 za mchongoko zimeshaagizwa na tayari 8 zipo nchini baadhi zinafanya safari na zingine zipo kwenye majaribio.
Pamoja na mambo mengine, Msigwa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika Stesheni ya SGR ya Jakaya Kikwete, Morogoro Januari 24, 2025.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇