LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 21, 2018

POLISI NCHINI YAAPA KUWASHUGHULIKIA WALIOMTEKA MO DEWJI

Baada ya kuachiliwa huru mfanyabiashara bilionea Mohamed Dewji aliyetekwa kwa takribani siku 9 jijini Dar es salaam, jeshi la polisi nchini Tanzania limeahidi kuwasaka na kuwatia nguvuni wahusika wa utekaji huo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro amewaambia waandishi wa habari kwamba, kuachiwa kwa Mohamed Dewji 'MoDewji' ni mwanzo wa kuwanasa wahalifu hao na kuahidi kwamba, jeshi la polisi litawapata wakiwa hai  au wamekufa.
Sirro amesema upelelezi umeimarishwa kwa kushirikiana na mtandao wa polisi wa kimataifa Interpol.
"Nataka niwaambie (wahalifu) yawezekana wananisikiliza hivi sasa kuwa, popote watakapoenda tutawanasa. Wakienda Afrika Kusini tunao, Kenya tunao, Uganda tunao hata Msumbiji, popote pale tutawakamata maana tayari tuna ushirikiano na wenzetu, alisisitiza IGP Sirro.
Kamanda Sirro amebainisha pia kwamba, mbio ukizianza sharti uzimalize. Huu ni mwanzo tu. Hao wahalifu wanaotaka kuchafua jina la nchi yetu lazima tuwatie nguvuni."
Mohamed Dewji, bilionea kijana
Aidha Kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la Polisi ambae pia ni kamanda wa kanda maalumu ya polisi Dar es salaam Lazaro Mambo Sasa amesema kuwa, kulingana na taarifa za hapo awali kwamba waliomteka Mohamed Dewji sio raia wa Tanzania, zimethibitishwa na Mo mwenyewe ambaye amesema wahalifu walikuwa wanatumia lugha inayofanana na lugha inayotumiwa huko nchini Afrika Kusini.
Mohamed Dewji maarufu kama MO Dewji alitekwa nyara na watu wasiojulikana alfajiri ya Alkhamisi Oktoba 11, 2018 na baada ya kushikiliwa kwa takriban siku tisa alipatikana jana na kuungana na familia yake.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages