Mganga wa Jadi aliyejulikana kwa jina la Moshi Hussen Rajabu aliyekuwa akiishi Kijiji cha Kwaga Wilaya ya Kasulu Tarafa ya Kasangezi alifika katika Kijiji cha Bitale Kigoma Vijijini kwa lengo la kusalimia ndugu na jamaa na alipofika nyumbani kwa Babu yake, Yatosha Nchiyiki katika kijiji hicho alikuta watu wakiongelea kuwa katika shamba lililopo eneo la Bolelo la aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho ndugu, Ezra Kabembo kuwa shambani kwake kuna nyoka ndio mganga huyo akasema kuwa yeye ni mganga na mtaalam wa kukamata nyoka, ndipo wananchi wakaongozana naye na kufika katika eneo la tukio, Ambapo alianza kujiandaa na nyoka ilimgonga mgonga huyo na mganga huyo alifanikiwa kukamata na kumuua nyoka huyo, hivyo mwili wa marehemu umesafirishwa leo Septemba 20, 2018 kuelekea kijijini kwao kwa mazishi ambapo yatafanyika 21, Septemba 2018.(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mwenyekiti wa Kijiji cha Bitale, John muyaya akionesha nyoka huyo baadhi ya wananchi waliofika nyumbani kwa mzee Yatosha Nchiyiki ambapo nyoka huyo alikuwa amehifadhiwa |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇