LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 18, 2018

DK. BASHIRU AWAFUNDA TBC KUHUSU UTANGAZAJI, LEO

                     
   TAARIFA KWA UMMA

Leo Tarehe 18 Septemba 2018, Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amefanya ziara ya kutembelea Shirika la Utangazaji Tanzania ( TBC) katika vituo vyake vya TAZARA na Mwenge Bamaga. Ndg Bashiru ameambatana  na mwenyeji wake Ndg.Ayoub Ryoba ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo pamoja na maafisa kutoka Chama Cha Mapinduzi.

Akiwa katika ziara hiyo Katibu Mkuu amepata fursa ya kuelezea hali ya kisiasa nchini ambapo,amesema mwenendo wa hali ya siasa nchini ni mzuri na kwamba vyama vya siasa vilivyoundwa kwa madhumuni ya kupata vyeo tu havitaweza kuhimili bali vile, vilivyoundwa kwa Itikadi madhubuti na vyenye shabaha ya kweli ya kuleta maendeleo ndivyo vitakavyoweza kuhimili joto la kisiasa nchini.

"Sisi ni Chama Cha Mapinduzi,Mapinduzi yaViwanda,Mapinduzi ya Kilimo,Mapinduzi ya Elimu,Mapinduzi ya Maisha kutoka kwenye kundi la watu wanaodhalilishwa na kuingiakatika kundi ambalo utu wao utathaminiwa.
Tukifanya hivyo vyama vile ambavyo ni vya mitambo ya uchaguzi na vyeo vitakufa, na vikifa tutakua tumevisaidia vile ambavyo vinakuja sasa kiitikadi na msimamo kusimama".Amesisitiza Ndg.Bashiru.

Aidha Ndg. Bashiru amefurahishwa na maudhui ya vipindi vya Shirika hilo na namna ambavyo limeweza kupanua mtandao wake wa upatikanaji wa masafa yao nchi nzima kwani limewarahisishia wananchi wengi kupata taarifa za ukweli na za uhakika kwa haraka zaidi.

Amewataka TBC kuendeleza kutoa 
vipindi vyenye kusisitiza Umoja ,Amani na Uzalendo wa Taifa, sambamba na historia ya viongozi waasisi kama vile hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, hayati Sheikh Abeid Karume na Waziri Mkuu hayati Edward Moringe Sokoine ili kizazi cha sasa kiweze kuelewa nchi hii ilipotoka ilipo na inapokwenda.

Imetolewa na,Idara ya Itikadi na Uenezi,
Chama Cha Mapinduzi,
OND -Lumumba

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages