Enzi za uhai wake marehemu Profesa Emil N Kikwilu 1950- 2018
Makamu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Prof. Andrea Pembe akizungumza na waombolezaji jana Septemba 30, katika viwanja vya chuo hicho kabla ya kutoa heshima za mwisho, ambapo alisem marehemu anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Kimara mwisho tarehe 31, Septemba
Makamu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Prof. Andrea Pembe nasikitika
kutangaza kifo cha Profesa Emil N Kikwilu kilichotokea usiku wa tarehe 27/08/2018. eneo la Kimara Dar es Salaam
Kabla ya kifo chake marehemu Emil N Kikwilu alikuwa Profesa katika Idara ya Afya ya Kinywa na Meno kwa Watoto na Jamii (Department of Orthodontics.Paedodonties and Community Dentistry) katika Skuli ya Afya ya Kinywa na Meno
Mipango na taratibu za mazishi zinafanyika na nyumbani kwa marehemu Kimara
Makamu Mkuu wa Chuo pamoja na Jumuiya ya MUHAS wanaungana na
familia ya marehemu Emil N Kikwilu katika kuomboleza msiba huo
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. amiin
IMETOLEWA NA:
OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO
YA UMMA-MUHAS. 28/08/2018
Dkt. Habiba Majapa akitowa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Profesa Emil Kikwilu
Rais mstaafu wa chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzani na Dkt, Bingwa wa Meno ya Watotowa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Rachel Mhavile akipita mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Profesa Emil Kikwilu
Mkuu wa Skuli ya Afya ya Kinywa na Meno (MUHAS), Dkt. Elison Simon (kushoto) akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Profesa Mhadhiri wa Skuli ya Meno Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Emil Namakuka Kikwilu nyumbani kwake eneo la Michungwani, King'ongo Kimara Dar es Salaam Agosti 31, 2018
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa profesa Emil N Kikwilu katika viwanja vya Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS)
Mhadhiri Skuli ya Meno Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Profesa Bakari Lembariti akipita mbele ya jeneza lenye mwili wa Mhadhiri Skuli ya Meno Chuo hicho, Profesa Emil N Kikwilu
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇