LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 6, 2017

KANALI MSTAAFU LUBINGA AMEKEA RUSHWA UCHAGUZI WA CCM TEMEKE

Na Dotto Nyirenda
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Kanal Ngemela Lubinga awahusi WANACCM na Viongozi wa Wilaya ya Temeke Mkoani Dar Es Salaam kuwa wasichague Viongozi Watoa Rushwa.
Ndugu kanali Lubinga ameyasema hayo Leo tarehe 06/10/2017 baada ya kualikwa na kuombwa kama Katibu wa NEC Idara ya siasa na uhusiano wa kimataifa(SUKI) kuwa mgeniRaami kabla ya kuanza Mkutano Mkuu wa CCM wa Uchaguzi wilaya ya Temeke ambapo alianza kwa kuwapa pole kwa misiba ya viongozi wawili wa CCM wa wilaya.
Baada ya hapo Kanali Lubinga aliwapongeza viongozi wa CCM wa wilaya ya Temeke kwa kuhakikisha mkutano huo unafanyika na maandalizi ya mkutano huo yanakamilika kwa wakati.
Ndg Kanali Lubinga aliendelea kusisitiza kwa wajumbe na viongozi waliohudhuria mkutano huo kuwa CCM mpya na Tanzania Mpya tofauti yake ni kwamba inafanya kazi katika spidi kubwa na kwa uweredi mkubwa sana kulingana na dunia ilivyo huku ikipinga vitendo vyote vya rushwa wakati huo huo ikihimiza maadili.
Aliendelea kusisitiza kuwa nguvu ya kufanikisha utekelezaji wa ilani ya CCM ipo mikononi mwetu sisi viongozi na wanachama wa CCM hivyo inapaswa kuelewa kuwa sote tumebeba dhamana ya watanzania zaidi ya Milioni 45 nchi nzima ambapo ni watoto, vijana, akinamama na wazee. Kikubwa kitakachofanya nchi yetu isiyumbe ni kusimama katika maadili na hii ni kwa wote viongozi na wanachama. Ndio maana CCM mpya inajengwa kwanza katika misingi ya maadili, haki, usawa na uwazi.
Hata hivyo Ndg Kanali Lubinga aliendelea kuwasisitiza wagombea na wajumbe wa mkutano huo kuwa tabia ya usaliti ndani ya Chama haitavumiliwa na hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa wanachama wasaliti.
pia aliendelea kuwasihi kuwa ambao kura hazitatosha siku ya leo waendelee kuwa mabalozi sahihi kwa Chama huku wakitetea Chama kila sehemu watakapokuwa.
Mwisho aliwasihi viongozi watakaopewa dhamana ya uongozi katika mkutano huo kwa nafasi mbalimbali tukianza na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya maana ndiye amebeba wilaya na ndiye anayepeperusha bendera ya CCM kwa wilaya ya Temeke
Hivyo tunategemea Mwenyekiti awaunganishe wanachama wote wa Temeke na viongozi kuanzia ngazi ya shina, kata, jimbo hadi hapo juu kwenye wilaya.
Mwisho alimalizia kwa kuwataka Mwenyekiti na katibu wa CCM wa wilaya kutambua nafasi zao katika kuwatumikia wanachama na wanapaswa kufanya kazi hiyo kwa ushirikiano wa hali ya juu ili viongozi wengine huku chini waige mfano.
Baada ya kusema hayo Ndg Kanali Lubinga aliwatakia wajumbe uchaguzi mwema wenye amani na utulivu

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages