LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 29, 2026

SERIKALI 'YAJITIA KITANZI' UJENZI WA BARABARA YA MLOWO - KAMSAMBA


Mbunge wa Mbozi, Onesmo Mkondya amezidi kuihoji serikali kwamba lini itamlipa mkandarasi malipo ya awali ya ujenzi wa barabara ya Mlowo – Kamsamba yenye kilometa 130 kwa kiwango cha lami?

Kwa niaba ya Serikali Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa alijibu kama ifuatavyo; Serikali imepanga kujenga Barabara hii kwa kiwango cha lami kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Mkataba wa ujenzi wa sehemu za Mlowo – Zelezeta (km 5) na Mkonko – Kamsamba (km 5) ulisaniwa mwezi Juni, 2025.

Kwa sasa, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya malipo ya awali ili mkandarasi aweze kuanza ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-0715264202

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages