Kihulla amewataka wafanyabiashara, hususan wanaonunua na kuuza mazao, kuachana na matumizi ya magunia, madebe, makopo, mafungu na vipimo vingine visivyo rasmi, akisisitiza kuwa mizani ndiyo njia sahihi ya kuhakikisha kiasi cha bidhaa kinapimwa kwa usawa.
“Madebe, makopo, visado na mafungu siyo vipimo, wafanyabiashara tumieni mizani,” amesema.
Amesema kilo ndiyo kipimo kinachotambulika katika biashara, hivyo matumizi ya mizani sahihi yanasaidia kuhakikisha muuzaji na mnunuzi wanapata haki yao bila mmoja kumdhulumu mwingine.
Amesema matumizi ya vipimo visivyo rasmi yanaweza kuleta tofauti kubwa katika kiasi cha bidhaa kinachouzwa na hivyo kusababisha kutokuwepo kwa usawa katika biashara.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇