LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 18, 2026

RAIS DK. MWINYI AMTEUA TENA OTHMAN MASOUD OTHMAN KUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua tena Mhe. Othman Masoud Othman kuwa Makamu wa kwanza ww Rais wa Zanzibar.


Taarifa ya Ikulu ya Zanzibar iliyosainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Mansura Kassim, imeandikwa kuwa, Uteuzi huo unaanza tarehe leo 18 Septemba, 2026.


"Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais ataapishwa siku ya Jumanne tarehe 22 Septemba, 2026 saa 4:00 asubuhi Ikulu, Zanzibar", imeandikwa taarifa hiyo.


Othman Masoud Othman, aliteuliwa kwa mara ya kwanza kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar tarehe 1 Machi 2021 na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi. Aliapishwa rasmi tarehe 2 Machi 2021.


Aliteuliwa kushika nafasi hiyo kujaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad tarehe 17 Februari 2021.



No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages