LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 27, 2026

WANANCHI KISWAGO WAMPA KONGOLE DKT. MDAKU UKAMILISHWAJI WA DARAJA

 Wananchi wa Kijiji cha Kiswago, Kata ya Sofi, Wilaya ya Malinyi, wametoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mhe. Dkt. Mecktridis Mdaku, kwa mchango wake wa Shilingi 500,000 uliochangia kufanikisha ukarabati wa daraja lililoharibiwa na mafuriko, na hivyo kurejesha matumaini ya wananchi.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema kukamilika kwa daraja hilo ni ushahidi wa uongozi unaowasikiliza na kuchukua hatua kwa wakati. Wameeleza kuwa sasa usafiri umerejea katika hali ya kawaida, watoto wanafika shuleni kwa urahisi, wafanyabiashara wanaendelea na shughuli zao bila vikwazo, huku wakimtakia Mhe. Mbunge afya njema na mafanikio zaidi katika kuwatumikia wananchi wa Malinyi.

Kwa niaba ya Mhe. Mbunge, Katibu wa Mbunge Ndugu Renatus Matola alitembelea eneo hilo na kujionea kukamilika kwa kazi ya ukarabati. Wananchi na viongozi wa kijiji wamepongeza ushirikiano huo wakieleza kuwa umeonesha dhamira ya dhati ya kutatua changamoto zinazowagusa wananchi.

Daraja hilo sasa limekamilika na tayari linatumika, likirejesha mawasiliano na kurahisisha usafiri wa wananchi pamoja na shughuli za kijamii na kiuchumi katika Kijiji cha Kiswago na maeneo ya jirani.







 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages