LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 23, 2026

WANANCHI WAMSHUKURU MBUNGE MDAKU KUCHANGIA UKARABATI WA DARAJA KISWAGO

Wananchi wa Kijiji cha Kiswago, Kata ya Sofi, Wilaya ya Malinyi, wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mhe. Dkt. Mecktridis Mdaku, kwa kuchangia Shilingi 500,000 zilizowezesha kuanza kwa ukarabati wa daraja lililobomoka kufuatia mafuriko na upepo mkali uliolikumba eneo hilo mwezi Aprili mwaka huu.


Shukrani hizo zimetolewa wakati Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Ndugu Renatus Matola, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa daraja hilo kwa niaba ya Dkt. Mdaku. 

Ndugu Matola amesema kwamba Mhe. Mbunge ameendelea kuweka mbele maslahi ya wananchi kwa kushiriki kutatua changamoto zinazogusa maisha yao ya kila siku, hususan miundombinu muhimu inayorahisisha huduma za kijamii na shughuli za kiuchumi.

"Dkt. Mdaku aliamua kutoa mchango huo mara baada ya kupata taarifa za uharibifu wa daraja hilo ili kuwasaidia wananchi kurejesha mawasiliano yaliyokuwa yamekatika kutokana na athari za mafuriko," 

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiswago, Ndugu Ndovu Matangiro, amemshukuru Dkt. Mdaku kwa kuguswa na changamoto ya wananchi na kuchukua hatua kwa wakati kwani mchango huo umeleta matumaini makubwa kwa wananchi na umewezesha kazi ya ukarabati kuendelea kwa kasi.

"Tunamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa kutusikia na kutuunga mkono, mchango wake umewezesha kazi kuendelea vizuri, na ninawahakikishia wananchi pamoja na Mhe. Mbunge kuwa ifikapo mwishoni mwa wiki hii ukarabati wa daraja utakuwa umekamilika," amesema Ndugu Matangiro.

Kukamilika kwa daraja hilo kunatarajiwa kurejesha huduma ya usafiri na mawasiliano kati ya maeneo mbalimbali ya kijiji, kurahisisha usafiri katika shughuli mbalimbali za maendeleo.









 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages