LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 29, 2026

RAIS WA TDA DK. BEREGE ASEMA UJIO WA RAIS WA FDI PROF. SHARKOV UMEWAONGEZEA CHACHU WANATAALUMA, AFYA YA KINYWA NA MENO

Na Khamis Mussa, Muhimbili
Rais wa Chama cha Madaktari wa Meno Tanzania (TDA) Dk. Gemma Berege, amesema ujio wa Rais wa Shirikisho la Madaktari wa Meno Duniani (FDI), Prof. Nikolai Sharkov umewaongezea chachu wao kama wanataaluma  na kuwafanya kudumu na kudumu zaidi katika misingi ya majukumu yao ya kila siku.

Amesema, ujio huo unawaongezea chachu kwa kuwa umegusa jukumu lao kubwa ambalo ni kulinda taaluma yao ikiwemo kwa kujiongeza katika elimu. "Tumefurahi kwamba hata katika mazungumzo yake Prof Sharkov, amesisitiza ushirkiano na kujituma, hivyo ametuongezea ari", alisema Dk. Berege.

Dk. Berege alisema pia ujio wa Prof Sharkov umeleta ari kwa vyama vya wanafunzi ambao kwa kuwa wamekuwa wakikutana naye kupitia wawakilishi wao na kupata ya kujifunza mengi kupitia kwake (Prof, Sharkov).

Kwa upande wake Prof, Sharkov ambaye alikuwa nchini na kupata fursa ya kukutana na viongozi wa TDA na Shule ya Tiba ya Meno ya MUHAS, aliwapongeza kwa mchango wao katika kuimarisha huduma za afya ya meno na kuzalisha wataalamu wenye sifa nchini Tanzania.

Pia amewahimiza wanafunzi wa tiba ya meno kuendelea kuwa makini katika masomo yao na kukuza taaluma zao ili waweze kuchangia ipasavyo katika mustakabali wa huduma za afya ya kinywa na meno.

Prof. Sharkov, alikutana na viongozi hao Mei 29, 2026, ambapo akiambatana na ujumbe wa TDA alitembelea MUHAS katika juhudi za kuimarisha ushirikiano katika elimu ya tiba ya meno na maendeleo ya taaluma hiyo.

Nyakati za mazungumzo na Prof. Sharkov, walihudhuria viongozi hao wa TDA, madaktari wa meno wa kada mbalimbali, wahadhiri wa MUHAS na wanafunzi kwa ajili ya kujadili fursa za ushirikiano katika mafunzo, utafiti, na kujengeana uwezo ndani ya sekta ya afya ya meno.

Dk. Berege akimpatia zawadi ya picha Prof Sharkov alipofika ofisi ya TDA.

Dk. Berege akimpatia zawadi ya fulana Prof Sharkov alipofika ofisi ya TDA.
Dk. Berege akimpatia maelezo kwa Prof Sharkov. kuhusu beji ya TDA kabla ya kumkabidhi.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages