LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 5, 2026

KATIBU WA CCM MKOA WA DSM COMREDI MKANDAWILE ALIPOONGOZA SEKRETARIETI YA MKOA KATIKA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA, UBUNGO, JANA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawire, mapema wiki hii alianza ziara na sekretarieti yake ya mkoa kuimarisha Chama, kwa kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, kuwasilisha Salam za Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwashukuru wanachama na wananchi kwa kuipatia CCM ushindi wa kishindo kwa Rais, Wabunge na Madiwani kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Katika ziara hiyo, pia aliweka amsha-amsha kwenyenye usimamizi na uratibu wa miradi mipya hasa katika sekta ya miundombinu na afya kulingana na utekelzaji wa Ilani na ahadi za CCM za Uchaguzi Mkuu wa 2025-30 na Chama kuanzisha miradi ya uchumi ili kijitegemee.

Pia katika ziara hiyo ambayo ililenga zaidi kupita katika mashina ya Chama, Mkandawire alitumia fursa hiyo kuonya wanaoanza kampeni za uongozi wa Chama kabla ya muda Uchaguzi utakaofanyika 2027.

Wakimpokea yeye na ujumbe wake katika shina namba 9,  tawi la Mpakani, mtaa wa Mpakani kata ya Kwembe na shina namba 5 Kata ya Makurumla lililopo Kata ya Makurumla, Ubungo, ilikuwa heka heka na pata shika nguo kuchanika, kwa Wanachama wa CCM kurindima kwa hoihoi na vigeregere.

Akiwa kwenye mashina hayo Mkandawire, alitumia uzoefu wake katika utendaji, kwa kusikiliza kero na baadhi yake kuzitatua papo hapo, ikiwemo kuamua kumpigia simu papo hapo Meneja wa mkoa wa Dawasa na kumuelekeza kutatua kero ya wakazi wa mtaa wa Mianzini ambao hawajapata maji ya bomba kwa miaka mitano sasa. Ziara hiyo ambayo ni ya Sekretarieti, kabla ya kuingia Ubungo, ilianzia Kigamboni na Ilala.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawire, akisaini kitabu cha wageni akiwa shina Namba 9,  tawi la Mpakani, mtaa wa Mpakani kata ya Kwembe wilaya ya Ubungo. Kushoto ni Mjumbe wa Shina hilo.
Wanachama wa CCM Shina Namba 9,  tawi la Mpakani, mtaa wa Mpakani kata ya Kwembe wilaya ya Ubungo, wakiwa tayari kumsikiliza Mkandawire.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawire, akipokea zawadi ya kitabu maalum kutoka kwa Mchungaji Joshua ambaye alimuombea kabla ya kumpa kitabu hicho.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawire, akifurahia watoto alipowasili shina namba 9.
Katibu wa Shina Namba tisa akisoma risala.
Wananchi shina namba 9
Wana CCM shina namba tisa wakishangilia ujio wa Mkandarire katika shina lao
Mwana CCM akieleza kero
Wana CCM wakiwa kwenye Mkutano shina namba 9
Wana CCM wakiwa kwenye Mkutano shina namba 9
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawire akipokea risala kutoka kwa Mwenyekiti wa shina namba 9
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawire akimsikiliza Mwenyekiti wa shina namba 9.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawire, akijadiliana jambo na Mwenyekiti huyo wa shina namba 9
Wana CCM katika shina namba 9
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawire, akizungumza na wanachama wa CCM katika shina namba 9, tawi la Mpakani, mtaa wa Mpakani kata ya Kwembe wilaya ya Ubungo.
Katibu wa CCM wilaya ya Ubungo Henry Msunga. 
Katibu wa CCM wilaya ya Ubungo Henry Msunga akizungumza kwenye mkutano ulifanyika shina hilo namba 9.
Katibu wa CCM wilaya ya Ubungo Henry Msunga  akisaidia kujibu baadhi ya hoja au kero katika shina namba 9. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawire akifuatilia kwa makini.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages