Serikali imejibu jumla ya maswali 3,318 kutoka kwa Wabunge katika Mkutano wa 3 wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao umehitimishwa tarehe 26 Juni, 2026.
Aidha, Katika mkutano huo Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amejibu maswali ya papo kwa papo 31. Kulikuwa na maswali ya msingi 696 na maswali ya nyongeza 2,591
Hayo yameelezwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa katika MKUTANO na Waandishi wa habari jijini, Dodoma Juni 28,2026, kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya wananchi.
"Katika mkutano huu, Bunge limepitisha bajeti ya kihistoria ya shilingi Trilioni 62.33 na limepitisha kwa asilimia 97.96. Hii ndio bajeti inayokwenda kuanza safari ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050."Amesema Msigwa.
"Halikadhalika katika Bunge hili Miswada miwili ya sheria imepitishwa na miswada mitatu imesomwa kwa mara ya kwanza. Lakini pia Bunge limetoa azimio la kuipongeza Timu ya Taifa ya Serengeti Boys. 

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇