LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 28, 2026

NMB, MASTERCARD WAZINDUA KADI MPYA KWA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WA KATI


 Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi (katikati), Mkurugenzi wa Mastercard anayesimamia biashara Afrika Mashariki, Imelda Ngunzu, na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Baraka Ladislaus, wakizindua rasmi kadi maalumu ya NMB SME World Business Credit Card jijini Arusha. 

                              ..........

Wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini wamepata fursa mpya ya kuongeza mtaji na kufanya malipo ya ndani na kimataifa, baada ya Benki ya NMB kwa kushirikiana na Mastercard kuzindua NMB SME World Business Credit Card jijini Arusha.


Akizungumza katika uzinduzi huo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema kadi hiyo inatoa mkopo wa hadi Sh50 milioni, kulingana na uwezo wa mteja, pamoja na kipindi cha hadi siku 53 bila riba endapo deni litalipwa ndani ya muda huo. Huduma hiyo itawawezesha wafanyabiashara kuongeza bidhaa, kulipa wasambazaji kwa wakati na kukabiliana na changamoto za muda mfupi za mtaji.


Mbali na huduma ya mkopo, kadi hiyo inaweza kutumika kupitia mtandao wa Mastercard duniani na ina manufaa yanayojumuisha bima ya matibabu ya safari ya hadi dola 100,000, bima ya mizigo, huduma za VIP Lounge katika zaidi ya viwanja vya ndege 400 na punguzo katika hoteli na huduma mbalimbali.


Mkurugenzi wa Mastercard anayesimamia biashara za SME Afrika Mashariki na Visiwa vya Bahari ya Hindi, Imelda Ngunzu, alisema kadi hiyo itasaidia biashara kupata mtaji kwa wakati na kufanya malipo kwa usalama. NMB pia itaendelea kuwekeza katika huduma za QR, PayByLink na mashine za POS ili kuboresha ukusanyaji wa mapato na ukuaji wa biashara katika uchumi wa kidijitali.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages