LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 13, 2026

UONGOZI WA TACAS WATINGA BUNGENI

 Viongozi wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TACAS), wamekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi  Seleman Kakoso bungeni Dodoma mwanzoni mwa wiki.


Wakiongozwa na Mwenyekiti wa TACAS, Ephrahim Rodrick Mwankusye waliwasilisha mbele ya kamati hiyo, baadhi ya kero ambazo walidai  zinasababisha Bandari ya Dar es Salaam kutojiendesha kwa ufanisi, kuelemewa na shehena ya mizigo na foleni ya meli za mizigo. 

Aidha, walitoa ushauri wa jinsi ya kutatua kero hizo kwa lengo la kuboresha uendeshaji wa Bandari hiyo muhimu kwa uchumi wa nchi na tegemeo kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu,Moshi Selemani Kakoso akiongoza kikao hicho.
Spika akikabidhiwa zawadi kutoka TACAS.




 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages