Mbunge wa Jimbo la Malinyi Mhe. Dkt. Mecktridis Mdaku ametoa msaada wa kuboresha mfumo wa usambazaji majisafi katika kituo cha Afya cha Kata ya Itete, Kilichopo Wilaya ya Malinyi, Mkoani Morogoro na kusaidia kuondoa adha ya upatikanaji wa maji iliyodumu kwa muda mrefu Kituoni hapo.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa changamoto hiyo kwa muda mrefu iliyoathiri utoaji wa matibabu kwa wagonjwa na wahudumu kushindwa kuhudumia vizuri.
Akizungumza wakati wa kukagua ukamilishwaji wa kazi ya kurekebisha mfumo wa maji katika kituo hicho, Mhe. Mbunge Mecktridis amesema kuwa kituo hiki cha afya kinafanya kazi kubwa ya kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa walio wengi wa Kata hii ya Itete, hivyo ukosefu wa maji katika Kituo hiki ni changamoto inyotishia na inayoathiri shughuli nzima za uuguzi kwa wagonjwa wanaokuja katika Kituo hiki.
"Hivyo, tumeona ni vyema kabisa kuweka mfumo huu wa upatikanaji mzuri wa huduma ya majisafi kwa lengo la kuwezesha utoaji mzuri wa huduma mahali hapa," amesema Mhe. Mecktridis.
Ameongeza kwa kumpongeza Mhe. Diwani wa Kata ya Itete Dr...Saulo kwa kuibua changamoto hii ya ukosefu wa maji katika kituo chicho na kuifikisha katika ofisi ya Mbunge kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi wa changamoto hii iliyodumu kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Daktari Kiongozi wa Kituo cha Afya Itete Dkt. Yusuf Nesta Mgeta amemshukuru Mhe. Mbunge kwa mchango wake wa thamani kwetu kwa kukikumbuka kituo hiki na kusaidia katika kuboresha mazingira ya utoaji tiba kwa wagonjwa.
"Kwa sasa maji katika kituo chetu yapo ya kutosha na huduma zinatolewa vizuri kabisa, tunamshukuru sana Mhe. Mbunge," ameeleza Dkt. Yusuf.
Naye Bi Janeth Godson mwananchi wa Itete ameishukuru ofisi ya Mbunge kwa kufanya jambo kubwa na la maana kwa kuweka maji katika kituo hicho na kusaidia sana kuboresha huduma nyingi.



No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇