Jimbo la Musoma Vijijini:
*Kata 21 zenye Vijiji 68
*Sekondari za Kata 30
*Sekondari Binafsi 2
*Sekondari mpya zinazojengwa 12
*High schools 3
*High schools mpya zinazojengwa 4
Leo, Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini imefanya kikao cha kugawa vifaa vya ujenzi vitakavyonunuliwa kwa kutumia Fedha za Mfuko huo.
Jumla ya Fedha: Tsh 75,796,000
Vipaumbele:
(i) Ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi (physics, chemistry & biology labs)
(ii) Ujenzi wa sekondari mpya za vijiji
MGAWO WA MIFUKO YA SARUJI:
Sekondari zinazojenga maabara:
1. Mtiro: mifuko 240
2. Nyanja: 200
3. Bukwaya: 200
4. Kigera: 200
5. Seka: 200
6. Tegeruka: 150
7. Suguti 50
Sekondari mpya zinazojengwa na vijiji:
1. Maneke: mifuko 100
2. Mmahare: 100
3. Nyambono: 100
4. Kastamu: 100
5. Musanja: 100
6. Chumwi: 100
7. Kataryo: 100
8. Kisiwa cha Rukuba: 100
MGAWO WA MABATI YA RANGI (gauge 28):
Sekondari zilizogawiwa
1. Mtiro: mabati 80
2. Mmahare: 76
3. Tegeruka: 75
4. Nyanja: 75
MGAWO WA NONDO (12 mm):
Sekondari zilizogawiwa
1. Nyanja: nondo 100
2. Tegeruka: 60
3. Suguti: 50
4. Mtiro: 40
5. Kigera: 30
Vifaa vyote hivyo vya ujenzi vitanunuliwa na Halmashauri yetu ndani ya wiki moja na kugawiwa kama ilivyopangwa.
Picha iliyoambatanishwa hapa:
Wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini wakiwa kwenye Kikao cha ugawaji wa vifaa vya ujenzi vitakavyonunuliwa kwa kutumia Fedha za Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini.
Mwenyekiti wa Mfuko huo ni Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo
SHUKRANI:
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuishukuru sana Serikali yetu, chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kugharamia miradi ya sekta ya elimu na ya sekta nyingine Jimboni mwetu - ahsante sana!
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Date: Fri, 13 March 2026

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇