Anaandika Yahya Msangi
Nina uhakika ni wakatoliki wachache nchini wanajua upapa uliwahi kuhamia Ufaransa kutoka Rome kabla haujarudishwa St Peters.
Pia najua ni wachache wamewahi kwenda kuhiji Ufaransa kwenye mji ambao makao makuu ya mapapa sana ulikuwepo. Mji huo unaitwa Avignon na uko Kusini mwa Ufaransa.
Je nini kilisababisha upapa uhame kutoka Rome kwenda Avignon (inatamkwa "avinyo")?
Palizuka mtifuano baina ya Mfalme Philip IV wa Ufaransa na Papa Boniface mapema mwaka 1300.
Mfalme alitaka kuongeza mapato yatokanayo na kodi ili kugharamia vita. Akaamua kuanza kutoza Kanisa kodi nchini Ufaransa na makoloni yake. Papa Boniface akapinga kwa madai kwamba Mfalme hana hayo mamlaka bila kupewa idhini na Papa. Papa akatoa Waraka (inajulikana kama Unam Sanctam) unaoharamisha kanisa kudaiwa Kodi bila idhini ya Papa.
Mfalme alichukia sana na akasubiri siku ambayo Papa alifanya ziara katika mji wa Anagni nchini Ufaransa akamkamata na kumtupa jela. Kikosi cha kijasusi cha Kanisa kikatumwa kutoka Roma kwenda kumkomboa. Kilifanikiwa kumkomboa lakini akafa siku chache baadae kutokana na mateso aliyopata akiwa jela.
Ndipo upapa wa Avignon ukaanza rasmi. Mapapa saba wakatawala kwa kipindi kirefu. Hii inajulikana kama "Babylon Captivity of the Church" aka "kutekwa kwa kanisa na watu wa Babylon".
Upapa huu ulikuwa mtiifu kwa wafalme wa Ufaransa. Ukipokea amri kutoka kwa Wafalme.
Kudumu kwa muda mrefu nchini Ufaransa kulichangiwa na kudhoofika kwa Dola ya Warumi nchini Italy.
Hali hii iliwaudhi wakatoliki wengi nje ya Ufaransa. Kwao Rome ndio makao ya St. Peters. Peter aliuawa (alisulubiwa kichwa chini miguu juu) na kuzikwa kwenye tundu la choo mjini Rome. Walipambana kurudisha upapa mjini Roma. Hatimaye wakipata Binti wa ukoo wa Mfalme (Catherine )wa Ufaransa aliyehimiza upapa kurudi Rome. Akamhimiza Pope Gregory IV aurejeshe upapa Rome.
Ukazuka mtafaruku! Rome wakateua Pope wakati kuna Pope mjini Asignon! Kanisa Katoliki likajikuta lina Mapapa wawili. Mmoja Mtaliano mwingine Mfaransa! Kanisa likaendeshwa kihivi mpaka kifo cha Pope Gregory IV ndio likarudi Rome na kuwepo Papa mmoja tu.
Ni jukumu letu tuliowahi kufika hadi Avignon na Rome kuwahabarisha ndugu zetu ambao hawaelezei hizi history. Wanafuata tu kama kondoo!

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇