LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 5, 2026

RAIS DK. SAMIA AFANYA UHAMISHO NA KUWAPANGIA VITUO MABALOZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uhamisho na kuwapangia vituo mabalozi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, mabalozi waliopangiwa vituo ni kama ifuatavyo.


(i) Balozi Togolani Edriss Mavura amepangiwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York;

(ii) Balozi Mhandisi Cyprian John Luhemeja amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Zambia;

(v) Balozi Dkt. Suleiman Haji Suleiman amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China;

(vi) Balozi Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Cuba, wengine walioteuliwa ni pamoja na
 
Balozi Salim Othman Hamad amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro;

Balozi Maulidah Bwanakheri Hassan amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman;

Pamoja na Swahiba Habib Mndeme amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Sweden. 


 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages