LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 26, 2026

KATIBU MKUU RAMEPRO,BONIVENTURA MWALONGO AKISAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO CHA MAREHEMU KARDINALI PENGO

Kwa masikitiko makubwa na huzuni nzito, tumepokea taarifa ya kifo cha Mwadhama Polycarp Cardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Marehemu alikuwa mchungaji mwaminifu na kiongozi mwenye hekima na busara, aliyelitumikia Kanisa na Taifa kwa uaminifu mkubwa, akiacha alama isiyofutika katika mioyo ya wengi.

Kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (TRAMEPRO), ninawasilisha salamu za rambirambi kwa Kanisa Katoliki, familia ya marehemu, waumini wote, na Watanzania wote walioguswa na msiba huu mkubwa katika Kanisa na Taifa letu.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, apumzike kwa amani ya milele.

“Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alikuwa kama sisi, nasi tutakuwa kama yeye; hivyo tujiandae.”

Imetolewa na:
Boniventura Mwalongo
Katibu Mkuu – TRAMEPRO

Tarehe: 24 Februari 2026


No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages