LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 25, 2026

PPAA IMEZUIA UTOAJI WA TUZO WA ZABUNI 43

 

Mamlaka ya Rufani  ya Zabuni za Umma (PPAA) Imezuia utoaji tuzo wa zabuni 43 zenye thamani ya kiasi cha TZS. 586,502,801,992/= kwa wazabuni waliokosa uwezo wa kifedha na sifa za kitaalamu zinazohitajika kutekeleza zabuni husika. 

Hilo limebainishwa na Katibu Mtendaji wa Mamlaka hiyo, alipokuwa akikelezea mafanikio ya Taasisi hiyo katika mkutano na waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mji wa Kiserikali, jijini Dodoma Februari 25, 2026.

"Hatua hii imezuia utekelezaji usioridhisha wa miradi, ambao ungesababisha upotevu wa fedha za umma na kuchelewesha maendeleo endelevu na stahiki kwa wananchi,"amesema 

 Aidha, katika baadhi ya mashauri hayo,   Mamlaka ya Rufani kupitia Sehemu ya Rufaa (Appeal Schedule) imefanikiwa kusajili mashauri takriban 196 yaliyotokana na michakato mbalimbali ya ununuzi wa umma ambayo baadhi ya hayo yamezuiwa.



"Serikali ya  Serikali ya Awamu ya Sita inaamini kuwa usuluhishi wa migogoro hauwezi kufanikishwa katika mazingira ya ubaguzi wala pale ambapo fursa na haki za kiuchumi na kiraia hazitolewi kwa usawa."amesema

"Kwa hivyo, hatua ya Mamlaka ya Rufani kuzuia utoaji wa tuzo kwa wazabuni 43 waliokosa sifa za kutekeleza zabuni, inaimarisha mchakato wa usuluhishi wa migogoro – moja ya falsafa nne 5 (4) za Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

mwaka 2023 Serikali ilitunga upya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023, ikifuatiwa na Kanuni za Ununuzi wa Umma za Mwaka 202

4 pamoja na Kanuni za Rufaa za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2025. Maboresho haya yameimarisha na kuleta ufanisi katika sekta ya Ununuzi na Ugavi kwa kuunganisha maeneo mengine ambayo kiutaalamu yanapaswa kuwa pamoja. Hapa ninazungumzia dhana nzima ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi (Supply Chain Management). Hii inahakikisha mnyoro mzima wa ugavi unasimamiwa kwa ufanisi, kuanzia upatikanaji wa bidhaa na huduma hadi usambazaji wa mwisho.




Waandishi wa Habari wakisikiliza kwa makini wakati wa mkutano huo.



Viongozi wa PPAA  


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203
 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages