LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 26, 2026

DK. MIGIRO: KADINALI PENGO AMEACHA PENGO KWA NAMNA YA MAISHA ALIYOISHI, CCM KUENZI MCHANGO WAKE KWA TAIFA.

Na Bashir Nkoromo, St. Joseph, Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Asha-Rose Migiro amesema Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo ameacha pengo kwa namna ya maisha aliyoishi ambayo yameacha alama ya kudumu miongoni mwa Watanzania.  

Amesema hayo, leo Februari 26, alipofika Kanisa la Mtakatifu Yosefu (St. Joseph), kusaini kitabu cha maombolezo na kuwasilisha Salamu za Rambirambi za CCM, kwa niamba ya Mwenyekiti wa Chama, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi OFMCap, kufuatia kifo cha Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo hilo, Kadinali Pengo, kilichotokea Februari 19, 2026, katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Dk. Migiro ambaye alifuatana na Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawili na viongozi kadhaa wa Chama mkoa huo, Kadinali Pengo atakumbukwa kama mchungaji wa faraja na tumaini, kiongozi wa kiroho mwenye hekima, unyenyekevu na msimamo thabiti wa maadili aliyejipambanua si tu kwa huduma ya Kanisa, bali pia kwa mchango wake katika kuimarisha mshikamano wa kitaifa, maadili ya jamii, malezi ya vijana na uwajibikaji. 

"Maisha yake ya imani, hekima na unyenyekevu yameacha alama ya kudumu mioyoni mwa Watanzania. Alikuwa mtu mwenye utulivu wa mawazo na kauli, mchungaji mwenye huruma, na sauti ya maadili ndani ya Kanisa na katika jamii. Aliamini katika amani, mshikamano na utu wa kila mwanadamu", alisema Dk. Migiro.

Alisema, katika miaka yake ya huduma kama Padre, Askofu na Kadinali, alijenga daraja kati ya imani na jamii, akisisitiza uimara wa familia, malezi ya vijana na uwajibikaji wa viongozi na alifundisha hayo zaidi kwa mfano wa maisha yake.

"Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, tunatambua na kuthamini mchango wake mkubwa kwa taifa letu. Urithi wake wa maadili na uongozi wa kiroho utaendelea kuwa dira kwa vizazi vijayo. Tunaliombea Kanisa na waumini wote wapate faraja katika kipindi hiki cha maombolezo. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Kwa hakika ameondoka duniani, lakini mwanga wa maisha na mafundisho yake utaendelea kuishi katika historia ya Taifa", alisema Dk. Migiro. 

Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akiwasilisha salam za rambirambi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hasaan, kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi OFMCap, kufuatia kifo cha Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo hilo, Kadinali Pengo, kilichotokea Februari 19, 2026, leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Stanley Mkandawile.

Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akiwasili kutoka Jijini Dodoma kwa Treni ya SGR kwa ajili ya kwenda kuwasilisha salam za rambirambi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hasaan, kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi OFMCap, kufuatia kifo cha Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo hilo, Kadinali Pengo, kilichotokea Februari 19, 2026, leo. Kulia ni mwenyeji wake, Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Stanley Mkandawile.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akiwasili kutoka Jijini Dodoma kwa Treni ya SGR kwa ajili ya kwenda kuwasilisha salam za rambirambi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hasaan, kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi OFMCap, kufuatia kifo cha Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo hilo, Kadinali Pengo, kilichotokea Februari 19, 2026, leo. Kulia ni mwenyeji wake, Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Stanley Mkandawile.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akilakiwa na Afisa Uhusiano wa Kanisa Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Cletus Magani, baada ya kuwasili kwa ajili ya kuwasilisha salam za rambirambi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hasaan, kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi OFMCap, kufuatia kifo cha Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo hilo, Kadinali Pengo, kilichotokea Februari 19, 2026, leo.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akishukuru wakati akilakiwa na Afisa Uhusiano wa Kanisa Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Cletus Magani, baada ya kuwasili kwa ajili ya kuwasilisha salam za rambirambi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hasaan, kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi OFMCap, kufuatia kifo cha Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo hilo, Kadinali Pengo, kilichotokea Februari 19, 2026, leo.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akielekezwa eneo la kwenda kusaini kitabu cha Rambirambi.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akisaini kitabu cha Rambirambi.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akisaini kitabu cha Rambirambi.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akitoa heshima baada ya kusaini kitabu cha Rambirambi.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akielekezwa kwenda ofisini kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi OFMCap, baada ya kusaini kitabu cha rambirambi.
Safari kwenda ofisini kwa 
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi OFMCap.
"Oooh! kumbe ofisi ipo pale", akasema Dk. Migiro.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi OFMCap, baada ya kuwasilini kwa Askofu Mkuu huyo.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akiwa katika mazungumzo na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi OFMCap, kabla ya kuwasilisha rasmi salam za rambirambi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hasaan. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Stanley Mkandawile.
Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile 'akifungua pazia' ili Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro awasilishe rasmi Salamu hizo za rambirambi.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akiwasilisha salam za rambirambi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hasaan, kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi OFMCap, kufuatia kifo cha Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo hilo, Kadinali Pengo, kilichotokea Februari 19, 2026, leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Stanley Mkandawile.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akiendelea na mazungumzo na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi OFMCap, baada ya kuwasilisha salam.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Asha-Rose Migiro akitoaka ofisini kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi OFMCap. Pamoja naye ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Stanley Mkandawile.
Katibu Mkuu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akimwelekeza Katibu Mkuu Dk. Migiro eneo la kuzungumza na Waandishi wa habari kuhusu yaliyojiri. Kulia mwenye shati la kijani ni Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo Ally Bananga.
Akizungumza na Waandishi wa habari.
Akiwa ameshaingia katika gari lake, tayari kuondoka baada ya kukamilisha ratiba hiyo ya kuwasilisha rambirambi na kusaini kitabu cha maombolezo.
Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Stanley Mkandawile akiagana na 
Afisa Uhusiano wa Kanisa Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Cletus Magani. Kushoto ni Adam Ngalawa wa CCM.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages