Vijana Mmemsikia Kaka Nape Nnauye?
Akizungumza na Clouds fm Nape amesema ‘Ushauri wangu kwa vijana uzoefu na historia inaonesha duniani Kote mahali ambako zimetokea vurugu za kisiasa, waliochochea, waliohamasisha na walioanzisha sio waathirika wakubwa, Wao na watoto wao wako salama ila waathirika wakubwa ni wale walioenda kufanya’ Nape Nnauye
‘Wito wangu kama kaka mkubwa vijana wasihamasike kwenda kufanya ambalo hawajui matokeo yake, kubwa kuliko yote namna yoyote ya kujaribu kuitoa serikali iliyoko madarani,hata kumtoa rais aliyeoko madarakani kinyume cha katiba ni uhaini,ujue watu wanafanya kama masihala na adhabu yake ni kubwa sana,tusimung’unye maneno na nchini kwetu kosa la uhaini adhabu yake ni kubwa sana ni kifo’ Amesema nape.
Aidha amesema kuwa ni muda wa kusubiri tume iliyoundwa na Rais ifanye uchunguzi na itoe majibu nini kilitokea na maada ya hapo tujadili lakini kwa sasa Tusikurupuke.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇