LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 5, 2025

JESHI LA POLISI LAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO DESEMBA 9

 

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limepiga marufuku maandamano yanayohamasishwa katika mitandao ya kijamii kwa kuyaita maandamano ya amani ya Disemba 09, 2025 kutokana na kutofuata taratibu kulingana na sheria ya Polisi pamoja na kujaa viashiria vingi vya uhalifu na uvunjifu wa sheria na taratibu.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Disemba 05, 2025 kwa Vyombo vya habari na msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime, imesema hatua hiyo imefikiwa pia kutokana na mbinu za kihalifu ambazo zimebainika wakihamasishana kuzitumia kuanzia tarehe 09 Disemba, maandamano hayo yamekosa aifa za kisheria kuyaruhusu kuweza kufanyika.

"Mtu yeyote anayepanga kufanya maandamano sheria inamtaka kuwasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa maandamano hayo kwa Afisa Polisi msimamizi wa eneo husika akiainisha sehemu yatakayofanyika maandamano hayo, muda, madhumuni na maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi mara kwa mara kwenye gazeti la serikali." Imesema taarifa ya Polisi.

Polisi pia imesema maandamano hayo yanakosa sifa kutokana na wanaohamasisha maandamano kuwa na silaha kwani wamekuwa wakiwataka waandamanaji ikiwa hawana mafunzo ya kutumia silaha asishike silaha siku hiyo bali awaachie wengine waliopata mafunzo ya kutumia silaha hizo.

Aidha waandamanaji pia wamekuwa wakihamasishana kupitia mitandao ya kijamii kuhakikisha kuwa bandari ya Dar Es Salaam haifanyi kazi, kufunga barabara zote za kuingia na kutoka nje ya nchi pamoja na kwenda kwenye Hospitali za umma na za binafsi kuzuia huduma za matibabu, suala ambalo ni kinyume na sheria za nchi.

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa watanzania na wasio watanzania ambao wapo ndani ya Tanzania wayakatae yanayohamasishwa na kutoshiriki katika maandamano hayo, wito ukitolewa pia kutoa taarifa kupitia namba 111, 112, 0699 998899 na 0787 668306 pale watakapoona tukio lenye viashiria vya uhalifu sehemu walipo.



 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages