Inua kichwa chako, wewe ni mwanaume, na Dunia ni uwanja wako wa vita.
Maisha ni kama mpira, ikiwa refa hajapuliza kipyenga cha mwisho, wakati wowote unaweza kuwaleta watu kati.
Ikiwa pumzi unayo, wewe ni kamanda, kiongozi mkuu, mbeba maono ya familia, mkata mnyororo wa Umaskini kwenye familia.
Ukikata tamaa wewe ni nani atafanya kama mbadala wako? Amka kamanda.
Pigana vita yako na ushinde mechi zako, hukuumbwa kumfurahisha kila mtu wala kupendwa na kila mtu, pambana kwa bidii kuishinda jana yako.
Kijana, adui wa kwanza ni akili yako, ukisema huwezi hautaweza kweli, ukisema unaweza basi kila kitu kitabaki historia.
Maisha ya uanaume sio marahisi, kuwa mwanaume ni gharama, lazima utailipia kupata heshima unayostahili, unatakiwa kuamini katika harakati zako, shabiki wa kwanza ni wewe mwenyewe.
Lia, cheka, anguka, vumilia, lakini hakuna kurudi nyuma.
Unaruhusiwa kupoteza lakini sio kushindwa, wape ushindi wanaokuamini, washangaze waliokuchorea mstari kwenye kilele chako, kila ukikaribia kukata tamaa kumbuka malengo yako, kumbuka watu waliopo nyuma yako, ikumbushe akili yako kuwa wewe ni mwalimu, mfalme, dunia imeumbwa kwa ajili yako.
Wewe ni bingwa, gwiji kabisa, askari ulietokea kijijini ambapo tumaini lao la mwisho ni wewe, usione aibu kuipambania ndoto yako na familia yako, vumilia dharau na matusi ya muda, wewe ni dhahabu unapitia kwenye moto kabla ya kupanda thamani.
Amini, ipo siku kama hawatakuheshimu wewe basi wataheshimu pesa zako.
Siku yako inakuja.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇