LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 3, 2025

KAMPENI ZA DKT SAMIA NI MWENDO MDUNDO MKOA WA MANYARA

 

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatinga Mkoa wa Manyara baada ya  jana Oktoba 2,2025 kufanya  Kampeni zake katika mkutano mkubwa kwenye Uwanja Sheikh Amri Abeid jiji Arusha.

‎Anaingia Mkoa huo baada ya asubuhi hii kuhitimisha kampeni Mkoa wa Arusha katika Wilaya ya Karatu na hatimaye mchana kuanza rasmi katika  wilaya ya Hanangu,

‎Baada ya kufanya uzinduzi wa kampeni kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe ijini Dar es Salaam Agosti 28, 2025, leo Oktoba 2, 2025 ameingia mkoa huo ukiwa ni Mkoa wa 20  baada ya kufanikisha kwa kiwango kikubwa kampeni katika mikoa mingine 19.

‎Tanzania Bara ni;  Morogoro, Dodoma, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Singida, Tabora, Kigoma, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

‎Tanzania Visiwani; Mkoa wa Kusini Unguja, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkoa wa Kusini Pemba.

‎Bado mikoa ya; Dar es Salaam,  Rukwa, Katavi, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mara, Kagera, Mwanza, Mkoa wa Mjini Magharibi na Mkoa wa Kaskazini Pemba

‎Akiwa katika mikutano hiyo, Dkt. Samia hujinadi kwa kuelezea mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika  mikoa hiyo, pia hutoa ahadi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.

‎Aidha, Dkt. Samia amekuwa akisisitiza kudumisha Muungano na kuendelea kulinda amani na utulivu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

‎Pia amewatoa wananchi wasiwasi kwamba hakutokuwa na vurugu  kwani vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko imara, hivyo siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu  wajitokeze kwa wingi tena bila hofu kwenda kupiga kura na kurejea salama majumbani.

‎Pamoja na kuelezea kwa undani Ilani ya uchaguzi ya chama hicho, Dkt. Samia ambaye mgombea wake mwenza ni Dkt. Emmauel Nchimbi, hutumia fursa hiyo kujinadi yeye,  wagombea ubunge na madiwani wa chama hicho.

‎IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203



 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages