Ni umati wa wananchi wa Kateshi mkoani Manyara waliojitokeza kwa ajili ya kuja kumlaki, kumsikiliza na kuahidi kumpa kura zake Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 leo tarehe 3 Oktoba 2025
Nyomi ya watu hawa imetokana na kazi kubwa iliyofanywa na uongozi thabiti wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 katika miaka 5 iliyopita na kazi hizo zimegusa maendeleo ya moja kwa moja kwa wana Katesh na Taifa kwa ujumla ndiyo maana unaona wamejitokeza kwa wingi huu kuja kumlaki na kusikiliza sera na ahadi za CCM kuelekea miaka 5 mingine.
Huu ni muendelezo wa mikutano ya kampeni za Urais kupitia CCM na sasa ni zamu ya mkoa wa Manyara, leo tarehe 3 Oktoba 2025.






No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇