LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 10, 2025

DKT. SAMIA ATIMIZA ASILIMIA KUBWA YA NDOTO ZA HAYATI NYERERE

  MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeweza kutekeleza miradi mikubwa ya utawala bora inayotoa msukumo kwenye sekta za uzalishaji ambayo ni sehemu ya ndoto ya Mwalimu Nyerere.

‎Ameyasema hayo alipokuwa akijinadi katika mkutano wa kampeni za CCM kwenye Uwanja wa Mwenge wilayani Butiama mkoani Mara Oktoba10, 2025. Nyerere aliizaliwa mwaka 1922 katika Kijiji cha Mwitongo wilayani humo.


‎Ameitaja miradi hiyo ni: utekelezaji mpango wa kuhamisha makao makuu ya nchi Dodoma."Tuliamua miaka ile kwamba makao makuu ya nchi yetu yatakuwa Dodoma, tumechelewa kidogo lakini kuanzia awamu ya tano na hii ya sita tumekamilisha uhamiaji wa serikali na kuifanya makao makuu iwe Dodoma.


‎Aliongeza: "Mihimili yote mitatu ya serikali tayari ipo Dodoma, Bunge lilitangulia, serikali tukafuata na Mahakama mwaka 2024 imehamia Dodoma."


‎Mgombea Urais Dk.Samia amesema jambo lingine ambalo lilikuwa ndoto ya Mwalimu Nyerere ni ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Julius Nyerere.


‎Amefafanua kwamba bwawa hilo alitaka lijengwe kipindi chake lakini hali haikuruhusu hata hivyo kwa sasa serikali imeshakamilisha ujenzi wa bwawa hilo.


‎“Mradi mwingine alioutaja ni mradi wa maji Same - Mwanga ambako alijenga bwawa la Nyumba ya Mungu lakini hakuweza kuuendeleza mradi huo.”


‎Amesema serikali imeundeleza na kuukamilisha mradi huo ambapo sasa wananchi wa Same, Mwanga na Korogwe wanafaidika na mradi huo.


‎Aliyataja mabwawa mengine ambayo Hayati Mwalimu Nyerere alitaka yajengwe ni bwawa la Mkomazi lililopo Korogwe ambalo limefikia asilimia 50 na bwawa la Kidunda ambalo lingesaidia maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na sehemu ya Morogoro.


‎Ameongeza bwawa hilo ujenzi wake upo asilimia 50."Zile ndoto za Mwalimu za utawala bora, sekta za uwezeshaji wananchi kiuchumi, maendeleo ya jamii ndiyo haya ambayo tunaendelea kutekeleza.


‎"Baba wa Taifa alituachia misingi mizuri kifalsafa, kisera na kisiasa. Kazi yetu ni kutafsiri misingi ile na fikra zile katika mazingira ya sasa," amesema na kuongeza Serikali itaendelea kudumisha tunu za amani, umoja, mshikamano wa taifa na muungano.





No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages