Na Richard Mwaikenda, Lamadi, Busega
Wananchi wa Lamadi wilayani Busega, Simiyu wamekiri mbele ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona kwa macho yao miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.
Wananchi walikiri kuiona miradi hiyo baada ya Dkt. Samia kutumia mtindo wa kuwahoji wananchi kama kweli wanashuhudia kuiona miradi ya afya, maji, elimu, umeme, barabara wilayani humo.
Kitendo hicho kilifanyika wakati wa mkutano wa kampeni za CCM Mjini Lamadi, Wilaya ya BUSEGA, mkoani Simiyu wakati Dkt. Samia aliposimama kuwasalimia na kuwaomba kura akielekea kuanza kampeni mkoani Mara.


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇