LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 9, 2025

IPENI KURA CCM INAYOJALI MASLAHI YA WANANCHI - DKT. SAMIA

 𝘼𝙨𝙞𝙨𝙞𝙩𝙞𝙯𝙖 𝙠𝙪𝙚𝙣𝙙𝙚𝙨𝙝𝙖 𝙣𝙘𝙝𝙞 𝙨𝙞 𝙟𝙖𝙢𝙗𝙤 𝙡𝙖 𝙢𝙖𝙟𝙖𝙧𝙞𝙗𝙞𝙤.


Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻, amewataka wananchi wa wilaya ya Bunda mkoani Mara na Watanzania wote kwa ujumla kutafakari kwa makini kabla ya kufanya maamuzi ya kisiasa katika kupiga kura na kuchagua Viongozi wawatakao.

Dkt. Samia ameweka msisitizo kuwa uongozi wa nchi unahitaji uzoefu na uwezo wa kusimamia masilahi ya wananchi.

Akizungumza katika muendelezo wa mikutano yake ya kampeni uliofanyika leo tarehe 9 Oktoba 2025, Dkt. Samia amesema uendeshaji wa nchi si jambo la majaribio, hivyo ni muhimu wananchi kuendelea kuamini chama chenye uzoefu wa kuongoza serikali na chama hicho ni CCM pekee.

“Ninataka niwaambie jambo moja kwamba katika uendeshaji wa nchi, hakuna majaribio."

"Unampa nchi yule ambaye unamuamini ataiendesha vyema na maslahi ya wananchi yatapatikana"

Aidha, Dkt.Samia ameongeza kuwa Chama Cha Mapinduzi kimekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya Watanzania wote ndiyo maana wameweza kutekeleza ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/25 kikamilifu, hivyo wananchi wanapaswa kuendelea kukiunga mkono ili kuwepo kwa safari ya maendeleo endelevu na kuinua utu wa kila Mtanzania.

Vilevile, amewasisitiza wananchi kutokubali kudanganywa na maneno ya vyama vingine vya siasa, akibainisha kuwa serikali inayoongoza ndiyo yenye mamlaka ya kupanga na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini na kutoichagua ni kusimamisha kama si kuua kabisa maendeleo ya nchi yetu.

Dkt. Samia amesisitiza hili;

“Mkiwapa wengine serikali au jimbo wanakuja kuwafuja, wanakuja kuwapoteza kwasababu wakiingia kwanza ni kujifunza, lakini utakapompa jimbo asiye Chama Cha Mapinduzi anakwenda kuongea na nani? Anakwenda kumuomba barabara nani? Anakwenda kumuomba maji nani? Kwasababu mwenye serikali ni Chama Cha Mapinduzi, yeye ni mpinzani"









 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages