Maelfu ya wananchi wa Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu wameonesha nidhamu na heshima kubwa katika kumpokea na kumkaribisha Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 leo tarehe 9 Oktoba 2025.
Dkt. Samia amewasili mkoani Simiyu ambapo atasalimiana na wananchi hao wa Lamadi, atanadi Ilani ya uchaguzi ya CCM (2025/30) , Sera na Ahadi zake ikiwa ni pamoja na kuomba kura kwa mafiga yote matatu yaani Rais , Wabunge na Madiwani.
Mara baada ya hapa, Dkt. Samia anatarajiwa kuendelea na mikutano yake ya kampeni za Urais ndani ya Mkoa wa Mara ambapo ataanzia wilayani Bunda.




No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇