May 24, 2025

RAIS DK. SAMIA AWAAPISHA VIONGOZI WAPYA, AWAPA TANESCO MAELEKEZO CHANYA

Ikulu, Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na uzalendo wakizingatia viapo vyao.

Ameyasema hayo leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam, alipokuwa akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, hafla mabayo ilihusisha pia kiapo cha maadili kwa viongozi waliokwishateuliwaa siku za nyuma.

Viongozi walioapishwa leo ni Prof. Tumaini Joseph Nagu kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Tawala za mikoa na Srikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya Afya, Dk. Blandina Buganzi Kilama kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshughulikia biashara na ubunifu, na Jaji Mstaafu John Samwel Mgetta kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili.

Rais amewataka viongozi hao kushirikiana kikamilifu katika kazi na watumishi wa ofisi wanazokwenda, kuheshimu maadili ya utumishi wa umma na kuwa mfano wa uongozi bora kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Pia Rais amewaagiza viongozi wa Tume ya Mipango kushirikiana katika uratibu wa miradi mikubwa ya kitaifa na kuhakikisha inafungamana na malengo ya kitaifa.

Kwa upande wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Rais amelielekeza kuelndeleza vyanzo vidogovidogo vya uzalishaji umeme nchini, kusimamia usambazaji wa umeme wa uhakika unaozalishwa na kutathmini uzalishaji umeme kwa vyanzo vya nishati jadidifu.

Rais wa Jamhusri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akihutubia baada ya kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, hafla mabayo ilihusisha pia kiapo cha maadili kwa viongozi waliokwishateuliwaa siku za nyuma, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Jaji Mstaafu John Samweli Mgetta kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Blandina Bugazi Kilama kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshughulikia biashara na ubunifu kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Prof. Tumaini Joseph Nagu kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya Afya kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2025.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages