CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinaanza kujenga jengo la kisasa la Makao Makuu jijini Dodoma mkabala na Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.
Jiwe la Msingi la ujenzi huo litawekwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Samia Suluhu Hassan Mei 28 mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM, CPA Amos Makalla, alipokuwa akuzungumza na vyombo vya habari jiji Dodoma Mei 24, 2025, kuhusu maandalizi ya Mkutano Mkuu maalumu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Mei 29-30 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.
CPA Makalla amesema kuwa Jengo hilo litakuwa la kisasa ambalo litakuwa na huduma zote muhimu na litaendana na hadhi ya CCM ambayo kwa sasa inawanachama zaidi ya milioni 11.
“Tunajenga jengo la Makao Makuu karibu na Jengo hili ( Jakaya Kikwete) ambalo litakuwa na facilities zote CCM ni Chama kikubwa Tanzania pamoja na Afrika,tumeona umefika wakati wa kuwa na jengo lenye facilities zote kumbi za mkutano, parking kwa sababu Chama hichi ni kimbilio la wananchi,”amesema Makalla.
Aidha, amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya Mkutano Mkuu maalumu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yamekamilika na unatarajiwa kufanyika Mei 29-30 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete na utahudhuriwa na wajumbe 2000 wa mkutano Mkuu kutoka mikoa yote nchini..
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makalla,akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇