Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), umetumia Sh.mil. 374 kufunga mtandao wa bure wa Intaneti maeneo ya wazi nchini kwa lengo la kuongeza wigo wa matumizi ya intaneti.
Hilo limeelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Peter Mwasalyanda wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habat MAELEZO jijini Dodoma Machi 27, 2025, kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mfuko huo kwa Kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inaoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan .
"UCSAF imefunga Public Free WiFi katika maeneo 7 na mengine 17 katika Viwanja vya maonesho ya Sabasaba Dar es Salaam, ili kuongeza wigo wa Intaneti," amesema Mwasalyanda.
Ametaja maeneo waliyofunga mtandao huo kuwa ni;
i.
Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha
Lungemba (Mafinga)
ii.
Nyerere Square (Dodoma)
iii. Ndaki ya Habari na Elimu Angavu (CIVE) Chuo Kikuu cha Dodoma
iv. Soko la Tabora (Tabora)
v.
Kiembe Samaki (Unguja) na
vi.
Soko la Buhongwa (Mwanza).
vii.
Maeneo Mengine 17 katika
Viwanja vya maonyesho ya Sabasaba
Aidha,Mwasalyanda amesema kuwa watafanya utafiti vijijini kubaini maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi kama vile kwenye masoko na kuweka mtandao wa Intaneti.
Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Peter Mwasalyanda wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇