Mar 25, 2025

MONGELLA ATOA WITO WA AMANI KWA WANACCM UCHAGUZI MKUU 2025

 Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu John Mongella, amewataka wanachama wa chama hicho kudumisha amani na utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Akizungumza Machi 24, 2025, jijini Arusha kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mongella amewahimiza wana-CCM kuwa makini na kuepuka vishawishi vinavyoweza kusababisha vurugu. Amesisitiza kuwa huu ni wakati wa kuwa imara, akibainisha kuwa Tanzania ina heshima ya kipekee barani Afrika kutokana na utamaduni wake wa kudumisha amani na utulivu.

Katika hotuba yake, Mongella ameipongeza Jumuiya ya Wazazi kwa kuandaa kongamano hilo la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutimiza miaka minne ya mafanikio katika uongozi wake.

Aidha, ameisifu jumuiya hiyo kwa mikakati yake madhubuti ya kukihami chama na kuhakikisha CCM inapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

    


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages