Mtandao wa Wana Blogu wa Tanzania (TBN) ni jamii yenye nguvu ya waendesha blogu wa Kitanzania walio ndani ya nchi katika Diaspora.
Ulimwengu wa blogu umekua kwa kasi, na blogu mpya inazaliwa kila sekunde, ikichangia katika hadithi inayobadilika ya jamii yetu.
TBN iliundwa rasmi Aprili 2, 2015, chini ya Sheria ya Tanzania ya Mashirika (CAP. 337 R.E. 2002) na kupata Cheti cha Usajili namba S.A. 20008 cha Tarehe 02 Aprili, 2015 kutoka kwa Msajili wa Taasisi zisizo za Kiserikali katika Wizara ya Mambo ya Ndani.
Uanachama wake wa awali ulianza na watu 100, ambapo baadaye walifikia 320. Makusudio mama yalikuwa ni kupanua TBN ili ijumulishe wanachama 1,000 wenye shughuli ndani na nje ya nchi miaka ijayo.
Masharti ya kuwa mwanachama ni kuwa na blogu yenye uhai usiopungua umri wa miezi sita.
Malengo:
Lengo kuu la TBN ni kuunganisha wana-Blogu wote wa Kitanzania wanaoishi nchini na walio katika Diaspora katika nyanja mbalimbali za kijamii, na kutoa jukwaa rasmi la kulinda maslahi ya pamoja.
Wakati huo huo, lengo ni kuweka nyenzo muhimu ya kutumikia Tanzania na watu wake kwa weledi.
Dhamira
Dhamira ya TBN ni kuhakikisha kuwa wanachama wake wanafanya kazi kwa maono yanayolingana na malengo makuu ya mtandao huu. Lengo letu ni kukuza weledi na athari ya tasnia ya blogu ndani ya jamii yetu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇