Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo - Hanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa shirika hilo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 26, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma. Pamoja na mambo mengine, Nyamo-Hanga amesema kuwa Tanesco wamo mbioni kuanzisha Mkoa maalumu wa SGR utakaokuwa na watendaji ambao kazi yao ya kila siku ni kuhudumia masuala ya umeme katika treni za SGR kwa lengo la kuhakikisha umeme huo unakuwa wa uhakika na madhubuti.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Zamaradi Kawawa akitoa neno la shukrani kwa uobgozi wa TANESCO na waandishi wa habari alipokuwa akihitimisha mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
Zamaradi Kawawa akimpongeza Nymo-Hanga baada ya mkutano huo kumalizika.
Zamaradi akimsindikiza Nyamo-Hanga.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇