Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu la Kimataifa (GPE), anaongoza vikao vya bodi ya taasisi hiyo jana na leo Jijini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Vikao hivyo vilifunguliwa
rasmi jana na Mhe. Reem Al Hashimy, Waziri wa Nchi wa UAE anayeshughulikia
Ushirikiano wa Kimataifa. Umoja wa Falme za Kiarabu umekuwa mshirika muhimu wa
GPE kwa miaka kadhaa.
Vikao hivyo
vinawakutanisha wajumbe wa bodi wakilisha wa nchi mbalimbali, mashirika ya
kimataifa, na vyama vya kiraia kutoka pande zote za dunia.
Miongoni mwa
wahudhuriaji mashuhuri alikuwa Mhe. Prof. Nasser Al Aqeeli, Naibu Waziri wa
Elimu wa Saudi Arabia, aliyeelezea dhamira ya Ufalme wa Saudi Arabia kuendelea
kushirikiana na GPE katika kutatua changamoto za elimu msingi (chekechea, elimu
ya msingi, na sekondari) katika nchi zinazoendelea.
GPEni mpango wa
kimataifa unaolenga kuboresha elimu katika nchi zinazoendelea, hasa kwa watoto
waliotengwa au wanaokosa fursa.
Ukiwa imeanzishwa mwaka
2002, GPE inasaidia elimu ya awali, msingi, na sekondari kwa kuzingatia usawa,
ujumuishi, na ubora wa masomo.
Shirika hili pia
huhamasisha rasilimali, kushirikiana na serikali, mashirika ya kiraia, na
taasisi za kimataifa, na hutoa ruzuku zinazolenga matokeo.
Tayari limebadilisha maisha ya mamilioni ya watoto katika nchi zaidi ya 90 kwa kuwapa fursa ya elimu bora na maendeleo endelevu.
Kulia kwa Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ni Mheshimiwa Prof. Nasser Al Aqeeli, Naibu Waziri wa Elimu wa Ufalme
wa Saudi Arabia. Kushoto kwa Mheshimiwa ni Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya GPE Christine Hogan na Mheshimiwa Waziri Reem Al Hashimy, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiongoza vikao vya bodi ya taasisi hiyo Jijini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu la Kimataifa (GPE), Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, katika picha za pamoja na wajumbe wa mikutano hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇