Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk, Hussein Ali Mwinyi ameisisitiza jamii kuendelea Kuitunza Amani iliopo wakati nchi ikielekea katika mwaka wa Uchaguzi Mkuu mwakani
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Waumini wa dini ya Kiislamu wa Masjid Shaafy uliopo Mombasa Mbuyu Mnene ,Wilaya ya Magharibi B.
Ameeleza kuwa ni wajibu wa Viongozi wa Dini na Wanasiasa kuwahubiria Amani waumini na wafuasi wao ili nchi iendelee kuwa na Amani na Utulivu na Serikali iendelee na mipango ya Maendeleo.
Aidha Alhaji Dk. Mwinyi amefahamisha kuwa kwa Miaka Minne nchi imekuwa na Utulivu Mkubwa wa kupigiwa mfano hali inayohitaji kuendelezwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Wakati huo huo Alhaj Dk. Mwinyi alifika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Lumumba kuwafariji na kuwajulia hali Wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo akiwemo Mzee wa Chama cha Mapinduzi Haji Machano.
Rais Alhaj Dk. Hussein Mwinyi akimjulia hali Mzee wa Chama Cha Mapinguzi (CCM) Mzee Haji Machano katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Lumumba, baada ya kutembelea wagonjwa wengine katika hospitali hiyo, leo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇