Katika kuhakikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji utakaofanayika taraehe 27 mwezi huu, unafanyika kwa ufanisi unaotakiwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, jana aliongoza mkutano wa wadau wa sekta ya habari ambao ulifanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa na wajumbe zaidi ya 200 ukihusisha Waandishi wa Habari, wadau wa habari, Makamanda wa Polisi wa mikoa, ulilenga kuwanoa wadau hao kuelekea Uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo baada ya kufunguliwa na Waziri Silaa mada mbalimbali zilitolewa na kujadiliwa na wadau.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa akifungua mkutano wa Wadau wa habari kuelekea Uchaguzi wa serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025, katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, jana. Zifuatazo ni baadhi ya taswira ya mkutano huo.👇
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇