LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 19, 2024

RAIS DK. SAMIA AONGEZA SAA 24 ZA UOKOAJI, "MWENYEZI MUNGU TUNAKUOMBA UTUFANYIE WEPESI KATIKA ZOEZI HILI", AOMBA RAIS DK. SAMIA

Na Bashir Nkoromo, CCM's Official Blog
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kuongeza saa 24 za uokoaji katika jengo lililoporomoka eneo la Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, Jumamosi, Novemba 16, 2029.

"Meshimiwa Waziri Mkuu, ninatambua utaratibu wa uokoaji una muda maalum wa saa 72 hadi kusitishwa. Binafsi nina matumaini kuwa Mwenyezi Mungu anaweza akatenda miujiza yake na kuweza kuwanausuru ndugu zetu wengine ambao bado wamenasa kwenye jengo hilo. Ninakupa maelekezo ya kutositisha uokoaji na kuongeza muda wa saa 24 zaidi ili kuwapambania ndugu zetu ambao tunaamini bado wako hai.

Kwa vikosi vyetu vyote na wananchi wote wanaopambana kuokoa maisha ya ndugu zetu katika kazi hiyo ya uokoaji naomba ufikishe salama zangu na uwaeleze kuwa natambua na nina wathamini sana. Wameonyesha utu, uzalendo mkubwa na uchapakazi wa hali ya juu sana. Hivyo nawatia moyo na kuwapa nguvu ya kuendelea kuwapambania ndugu zetu kwa kuwa ni mashujaa wa taifa letu", Rais Dk. Samia ametoa maelekezo na kusema hayo wakati akizungumza na Waziri Mkuu kwa njia ya simu akiwa nchini Brazil kikazi.

"Rais Dk. Samia anawaombea kwa Mungu awalinde na kuwapa nguvu muda wote wakiwa wanatekeleza jukumu hilo kubwa na kizalendo.

Rais Dk. Samia amewasilihi wananchi, ndugu na jamaa kuendelea kuwa na subira na kama taifa tuendelee kuwaombea ndugu zetu na wapiganaji wetu ili tufanikishe zoezi hili kwa mafanikio makubwa.

Mwenyezi Mungu tunakuomba utufanyie wepesi kwenye zoezi hili. Amina." Rais Dk. Samia amesema na kumuomba Mungu, katika taarifa iliyotumwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga, leo.

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages