LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 19, 2024

CCM KUKIWASHA KESHO UZINDUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, VIONGOZI WATAWANYWA MIKOA YOTE, BALOZI DK. NCHIMBI KUUNGURUMA MWANZA, MAKALLA DAR ES SALAAM

Na Bashir Nkoromo, Blog ya Taifa ya CCM
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kesho, Jumatano Novemba 20, 2024, kitazindua kwa kishindo nchi nzima kampeni zake za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na vitongoji, Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, akiongoza ufunguzi wa kampeni hizo kwa kufanya mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Furahisha, Nyamagana, jijini Mwanza.

Wakati Balozi Dk. Nchimbi ambaye pia ni mlezi wa kichama wa mkoa wa Mwanza akiunguruma katika mkoa huo, Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, ambao ni walezi wa mikoa mingine, na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, watazindua kampeni hizo kesho hiyo hiyo katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, kila mmoja akiwa katika mkoa aliopangiwa.

Taarifa ya Makao Makuu ya CCM, imesema Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Mongella, atakuwa mkoani Mbeya, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk. Mohamed Said Dimwa -Katavi, Katibu wa NEC Oganaizesheni  Issa Haji Usi Gavu - Geita na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi  Amos Makalla- Dar es Salaam.

Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) - Kilimanjaro, Makamu wa Rais Dk. Phillip Mpango - Dodoma,  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa - Kigoma, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar  Hemed Abdulla Suleiman - Tanga, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zuber Ali Maulidi - Singida na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda - Arusha.

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo - Mtwara, Halima Mamuya - Njombe, Nasir Ally Juma - Tabora, Mohamed Aboud Mohamed - Iringa, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mohamed Ali Mohammed (Kawaida) - Morogoro, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Fadhili Mgaya - Simiyu na Naibu Waziri Mkuu Dk. Dotto Mashaka Biteko - Mara.  

Wengine ni Hussen Bashe - mkoani Shinyanga, Livingstone Lusinde - Manyara, Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Ally Hapi - Kagera,
Nape Nnauye - Rukwa, Zainab Shomari - Lindi, Salim Faraji Abri (Asasi) - Ruvuma, Katibu Mkuu wa UVCCM  Jokate Mwengelo - Pwani na Richard Kasesela - Songwe.  

Taarifa imesema mkakati huo wa kuzindua kampeni kwa mtindo wa ushirikiano wa karibu viongozi wakuu na wanachama unaonesha jinsi CCM inavyothamini uchaguzi wa Serikali za Mitaa na udhihirisho wa dhamira ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya vyama vya upinzani, ambavyo hadi sasa vimeshindwa kusimamisha wagombea wa kutosha kushindana kikamilifu.

Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi kuongoza uzinduzi wa kampeni za CCM kesho, Uchaguzi Serikali za mitaa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages