LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 22, 2024

WABUNGE MOSHI VIJIJINI WASHIRIKI KUKABIDHI MIKOPO YA SH. 141 KWA VIKUNDI 10

 Wabunge wa majimbo ya Moshi Vijijini (Profesa Patrick Ndakidemi) na wa jimbo la Vunjo (Dr Charles Kimei) na wale wa viti maalumu mkoa wa Kilimanjaro Waheshimiwa Shally Raymond na Esther Maleko walishiriki katika hafla ya kutoa mikopo kwa vikundi kumi katika  Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro. Hafla hiyo, ilifanyika Novemba 20, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, eneo la KDC.


Mikopo yenye thamani ya Sh milioni 141.8 ilitolewa kwa vikundi 10 vilivyohusisha akina mama na  vijana katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa serikali wa 2024/25. Katika mikopo hiyo,  Sh milioni 74,182,000 zilitolewa kwa vikundi 6 vya wanawake na jumla ya Sh milioni 67,500,000 kwa vikundi vinne vya vijana.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wabunge hao waliipongeza serikali kwa kuifungua upya mikopo hiyo ambayo wamesema ni fursa itakayowawezesha wananchi kujiendeleza kiuchumi na kujikwamua kimaisha. Waliwashauri wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia kwa malengo yaliyowekwa na pia wairudishe kwa wakati ili iweze kunufaisha wananchi wengi.


Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini alishauri wawezeshaji waweke nguvu kwenye kuwaelimisha vijana wa kiume ili waitumie vyema fursa hiyo kwani uwakilishi wao ulikuwa mdogo sana.


Akikabidhi mikopo hiyo Mkuu wa Wilaya ya Moshi James Kaji ametoa wito kwa waliokopa mikopo hiyo kuitumia kama inavyotarajiwa. Aliwaelekeza maafisa ustawi wa jamii walioko Halmashauri ya Moshi watoe elimu kwa watu wenye ulemavu ili nao waweze kunufaika na mikopo hiyo


Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi (wa pili kulia) akishiriki kukabidhi mfano wa hundi hiyo.

Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi akizungumza baada ya kukabidhi mikopo hiyo.

Mbunge wa Vunjo, Dk, Charles Kimei akitoa neno wakati wa hafla hiyo.

Baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages