Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC), Salim Abri Assas, ameweka wazi mikakati ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa mwaka 2024, akibainisha kuwa vituo vyote 87,000 vya kupigia kura nchi nzima vitakuwa na sanduku la kura, hata katika maeneo ambayo hayana wagombea wa vyama vya upinzani.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni mkoani Ruvuma, Assas alisisitiza umuhimu wa wanachama wa CCM kushiriki kwa wingi katika mchakato wa uchaguzi. “Tutahakikisha kila kituo kina sanduku la kura, na pale ambapo hakuna wagombea wa upinzani, wapiga kura watapiga kura za ndiyo kuwachagua viongozi bora wa CCM,” alisema.
Katika hotuba yake, Assas alisisitiza umuhimu wa mshikamano wa wanachama wa CCM, akieleza kuwa mafanikio ya chama hicho yanatokana na juhudi za pamoja za wanachama wake. “Tunataka kuhakikisha viongozi wanaochaguliwa wanadumisha misingi ya maendeleo na mshikamano wa kitaifa,” aliongeza.
MNEC Assas alitumia fursa hiyo kuhimiza wananchi kuendelea kuamini katika CCM kama chama chenye dira ya maendeleo, akitaja miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa nchini kuwa ushahidi wa mafanikio yao.
Wanachama wa CCM waliojumuika kwenye mkutano huo walionyesha shauku kubwa, wakiahidi kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuwa mtetezi wa maendeleo ya taifa.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC), Salim Abri Assas, akivishwa skafu
Assas akipokea kadi na bendera za upinzani waliohamia ccm.
Asas akihutubia katika mkutano huo na kuweka wazi mikakati ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa mwaka 2024, akibainisha kuwa vituo vyote 87,000 vya kupigia kura.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇