LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 23, 2024

MAKALLA: CCM HATUCHEKI NA MTU KATIKA KUSHIKA DOLA,TUMEJIPANGA KUSHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Kibamba, Dar es Salaam
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ( NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Itikadi na Uenezi, CPA Amoss Makalla amesema CCM imejipanga kuhakikisha inashinda kwa kishindo Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu, na kwamba haicheki na mtu katika kushika dola.

CPA Makalla ameyasema hayo leo Movemba 23,2024 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 mwezi huu.

Amesema kwa sasa CCM imeendelea kufanya kampeni za Uchaguzi ambazo ilizizindua rasmi juzi, Novemba 20 katika mikoa yote nchini na tangu kuanza kampeni hizo wagombea wa CCM wataibuka na ushindi wa kishindo .

"Katika uchaguzi huu wa Serikali ya Mitaa tutashinda na tunataka ushindi wa kishindo. Kwa jinsi ambavyo CCM tumejipanga ni sawa na kusema yanayoendelea ni sawa na kusema yajayo yanafurahisha,"amesema CPA Makalla.

Akisisitiza zaidi amesema uchaguzi huo ni muhimu na CCM inachukulia uchaguzi huo kwa umuhimu mkubwa kwani inatambua kazi ya chama cha siasa ni kushika dola na Chama hicho kinaanza na kushinda uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

"Kazi ya Chama cha siasa kilichosajiliwa ni kuhakikisha kinashika dola maana kazi ya kuhubiri kwenda mbinguni hiyo inafanywa na viongozi wa dini.Kwa kutambua umuhimu wa kushika dola ndio maana katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa CCM imeweka wagombea wake kwa asilimia 100 kwani hakuna Mtaa,Kijiji Wala Kitongoji ambacho tumeacha,kote tumesimamisha wagombea a kwa nafasi zote.

"Vyama vingine havina utayari na ndio maana wameshindwa kusimamisha wagombea katika nafasi zote na mpaka sasa kuna Mitaa ambayo tayari wagombea wake hawana washindani,"amesma CPA Makalla na kuongeza katika maeneo ambayo wapinzani hawajasimamisha wagombea kampeni ziendelee maana kutakuwa na ndio au hapana.

Hata hivyo amesema katika maeneo ambayo wapinzani hawajasimamisha wagombea wamepanga kupiga kura ya hapana lakini akiwaangalia haoni kama wanaoubavu huo kwani kama wameshindwa kuweka wagombea ubavu wa kuzuia wagombea wa CCM wasishinde wanaoutoa wapi.

"Kwa wapinzani wanaofikiri wanaweza kuiangusha CCM kwa kura za hapana ni sawa na kusubiri meli katika uwanja wa ndege ni jambo ambalo haliwezekani."

CPA Makalla amesema kampeni za uchaguzi huo zimebakisha siku tatu lakini amesisitiza kwamba kama ambavyo wamezindua kampeni kwa kishindo na watafunga kampeni kwa kishindo na katika hilo wamejipanga vizuri.

"Tangu tulipozindua kampeni, zinaendelea vizuri na maelfu ya wapinzani wanarudi CCM na kuna wagombea wa vyama vingine na wenyewe wanataka kujiunga na CCM".

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CPA Amos Makalla akihutubia mkutano wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Kibamba Jijini Dar es Salaam, leo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages