LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 23, 2024

UMOJA WA VYAMA VYA SIASA KIGOMA WAIPONGEZA SERIKALI KUFANIKISHA VYEMA UANDIKISHAJI

Umoja wa Vyama vya Siasa mkoani Kigoma, umeonesha kuridhishwa na namna ambavyo Serikali mkoani Kigoma ilivyosimamia utekelezaji wa zoezi la uandikishaji wa daftari la orodha ya wapigakura kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa Serikali za vijiji na Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.


Mwenyekiti wa Umoja huo, Ramadhani Kasongo amesema wakati zoezi likiendelea wamefanikiwa kutembelea kwenye halmashauri na kujionea hali ya utekelezaji wa zoezi hilo ambapo wameridhishwa na ushirikishwaji mkubwa wa vyama vyote vya siasa katika maamuzi yaliyokuwa yakifanywa na wasimamizi wa uchaguzi huo.


Aidha Kasongo ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendesha zoezi hilo kwa uwazi huku akito wito kwa wanachama wa vyama vyote vya siasa mkoani Kigona pamoja na wasimamizi wa uchaguzi huo kuendelea kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za uchaguzi wa Serikali za Mitaa hali itakayochangia wananchi kupata viongozi bora watakaosimamia maendeleo yao.


Naye Katibu wa Chama Cha NCCR-Mageuzi mkoa wa Kigoma Rajab Nyambaro ametoa wito kwa makatibu wa vyama vya Siasa  mkoani Kigoma kuendelea kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo kupitia kutoa hamasa, kusimamia maadili ya vyama vyao pamoja na kufuatilia hatua zote za uchaguzi  ili kuondoa sintofahamu zinazojitokeza kuhusu zoezi la uchaguzi miongoni mwa wanachama wao.


Upande wake  Katibu wa Chama cha Ada -Tadea Musa Nkumila, amesema lengo la ukaguzi uliofanywa na viongozi hao ni kutaka kujiridhisha na maendeleo ya zoezi hilo sambamba na kutoa hamasa kwa wakazi wa mkoa wa Kigoma katika maeneo waliyoyafikia.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Kigoma, Ramadhan Kasongo akielezea katika mkutano wao jinsi walivyoridhishwa na mchakato huo wa uandikishaji. Kushoto ni Katibu wa NCCR-Mageuzi wa mkoa huo, Rajab Hamis.

Baadhi ya viongozi wa vyama wakiwa katika mkutano huo.





No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages